Fungua akaunti automatic ili uanze kuchati na kulipwa moja kwa moja.
LicoChat ni jukwaa la kidijitali linalowaunganisha watu wanaotaka kujifunza Kiswahili na wale wanaotaka kufundisha au kuzungumza Kiswahili kupitia mazungumzo ya mtandaoni. Kupitia jukwaa hili, wanachama wanaweza kujenga ujuzi wa lugha huku wakipata fursa ya kuingiza kipato kwa muda wanaotumia kwenye mazungumzo.
Kuwa jukwaa linaloaminika zaidi la kujifunza na kufundisha Kiswahili mtandaoni Afrika Mashariki, kwa kuhakikisha uwazi, usalama, na malipo ya uhakika kwa wanachama wetu wote.
Una swali, malalamiko, au unahitaji msaada? Timu yetu iko tayari kukusaidia kupitia njia mbalimbali za mawasiliano.
Karibu LicoChat. Masharti na Sheria hizi (โMashartiโ) zinaeleza jinsi unavyoweza kutumia huduma zetu kupitia tovuti licochat.site au njia nyingine yoyote inayohusiana. Kwa kutumia huduma zetu, unakubali Masharti haya yote. Kama hukubali, tafadhali usitumie huduma.
Ili kutumia LicoChat, lazima uwe na umri wa miaka 18 au zaidi, au umri wa kisheria wa kufanya mikataba katika nchi yako. Kama huna umri huo, hutakiwi kujisajili wala kutumia huduma.
Huruhusiwi kutumia LicoChat kwa:
Ukiukaji wa kanuni hizi unaweza kusababisha kusimamishwa au kufutwa kwa akaunti yako bila taarifa ya awali.
Unabaki na umiliki wa maudhui unayounda na kutuma kupitia LicoChat. Hata hivyo, unatupa leseni ya kutumia, kuhifadhi, na kuchakata maudhui hayo kwa madhumuni ya kuendesha na kuboresha huduma. Tunahifadhi haki ya kuondoa maudhui yanayokiuka Masharti haya.
Sheria za malipo, njia za malipo, muda wa kuchakata, na masharti ya withdrawal zimeelezwa kikamilifu kwenye Sera ya Malipo na Withdrawal. Kwa kutumia huduma, unakubali sera hizo.
Tunaweza kusimamisha au kufuta akaunti yako endapo:
Unaweza pia kuomba kufuta akaunti yako mwenyewe kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa wa mawasiliano.
Huduma za LicoChat hutolewa โkama zilivyoโ na โkama zinapatikana.โ Hatuahidi kiasi maalum cha mapato. Mapato yanategemea muda wa mazungumzo, makubaliano na mteja, na mambo mengine yasiyodhibitiwa nasi. Hatuwajibiki kwa hasara yoyote isiyo ya moja kwa moja inayotokana na matumizi ya huduma.
Masharti haya yanaongozwa na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Migogomo itatatuliwa kwa mazungumzo ya kindugu kwanza. Kama ikishindikana, itapelekwa kwa vyombo vya kisheria vya Tanzania.
Tunaweza kusasisha Masharti haya muda wowote. Tutaarifu kuhusu mabadiliko makubwa kupitia tovuti au barua pepe. Kuendelea kutumia huduma baada ya mabadiliko kunamaanisha unakubali Masharti mapya.
| Njia | Maelezo |
|---|---|
| M-Pesa | Malipo kupitia akaunti ya M-Pesa ya Tanzania. |
| Mix by Yas | Malipo kupitia Mix by Yas. |
| Airtel Money | Malipo kupitia Airtel Money. |
| Halopesa | Malipo kupitia Halopesa. |
| NMB / CRDB / NBC | Kwa maombi maalum; gharama za benki zinabebwa na mtumiaji. |
Njia nyingine zinaweza kuongezwa baadaye. Taarifa zitahuishwa kwenye ukurasa huu.
| Hatua | Muda |
|---|---|
| Maombi ya withdrawal | Siku 1โ3 za kazi |
| Uthibitisho wa akaunti (KYC) | Hadi siku 2 za kazi |
| Malipo kufika | Hadi siku 1โ2 baada ya idhini |
Kama hujapokea malipo ndani ya muda uliotajwa, wasiliana nasi kwa tosanduju01@gmail.com ukiambatanisha:
Tutajibu ndani ya siku 3โ5 za kazi.
Malipo yaliyokwisha kuchakatwa hayarudishwi isipokuwa kama kuna hitilafu ya kiufundi iliyothibitishwa na timu yetu. Maombi ya refund yanapaswa kutumwa ndani ya siku 7 tangu tarehe ya malipo.